Tuesday, July 31, 2007

wame kazalisha na haka duh


Duniani kuna mambo jamani hivi waweza kusema labda mtoto huyu amepewa mdogowake amshike.Kwa akili ya kawaida mzazi anaye weza kumpa mtoto mdogo kama huyu abebe kichanga kama hicho inawezekana hana uchungu na mwanae. lakini mtoto huyu si tu kama amembeba mtoto mwenzake bali amezaa mtoto mwenzake, haya yametokea uko kericho Kenya kwa mtoto wa miaka kumi aliekuwa akisoma shule ya msingi chemamul. naona haya ni baathi ya maajabu ya East Africa.

Thursday, July 26, 2007

Egidio toa maoni kaka


Enzi hizooooooo,kaka kitururu naomba unitaftie mashairi ya fool again,yataleta maana apa!

mabingwa wa rivas


hadi kwenye sehemu muhimu kama hizo, apo anamaanisha STOP, sasa mwanawani ukipitiliza inakuwaje? duh!

hatari! hatari!hatariiiiiiii!1


wapi hapa jamani!! hapa ni hatari kuliko pale kwa bwana egidio ina kuwajehapo jamaa akiparamia nguzo hilo?

Wednesday, July 25, 2007

duh mambo manane musiyoyajua kuhusu mimi

kaka kitururu kani tag na kaniomba mambo nane muhimu wasiyojulikana kuhusu mimi.
labda la kwanza nihili na ingawa silipendi lakini ninalo, sijui kukasirika ingawa nauzika,kuonyesha hali ya kukasirika nashindwa nabaki naumia moyoni.
napenda muziki, napenda kuimba ila siwezi kushika mashairi,
napenda usingizi ila sipendi kulala,
sipendi kung'atwa na mbu ila ni mvivu wa kushusha net,
nina huruma sana,
kupiga kibuti siwezi, napataga shida sana hapa ila napenda kukutanamarafiki wapya,
napenda sana pombe ila sipendi kulewa,
napenda kuandikiwa barua , sms kwenye simu ila mvivu kujibu.
ayo ni baathi tu ya yale ambayo amyajui kuhusu mimi, ok namimi naomba niwakandamizie na mimi nana watuambie mambo nane tusiyo yajua kuhusu wao
wa kwanza ni
1.mjegwa
2.mwaipopo
3.chedieli
3.luihamu
4.damija
5.chemi chemponda
6.da'mija
7.father kidevu
8.miruko
nawasubiria kwa hamu wandugu!

Thursday, July 19, 2007

simu za mkononi na masharti yake

wanasema tutumie sikio la kushoto kusikilizia simu za mkononi, wakimaanisha kuna madhara ya kutumia sikio la kulia kwa matumizi hayo, bado haijaniingia akilini, naomba kufaamishwa,
nawasilisha

Thursday, July 05, 2007

TEMBO WA NGORONGORO

Tanzania tumejaliwa vivutio vingi vya asili lakini bado atujafaidi matunda yatokanayo na mazao haya ya asili.