Saturday, January 31, 2009

malalamiko ya wanazuoni idara ya sociologia UDSM

Kuna mambo mengi yanayoendelea katika elimu ya juu katika nchi yetu, kama wewe ni mwanadhuoni na hukuwahi kupatwa na msukosuko wa kupata suplimentary katika masomo yako nakupa hongera sana na itakuwa vigumu kuwaunga mkono baadhi ya hawa wanaolalamikia matokeo yao katika harakati za kujikwamuo katika elimu zao. kunamalalamiko mengi katika vyuo vyetu.kuna baadhi ya wahadhiri wanaamini kufelisha wanafunzi ndio kipimo cha elimu bora, sitaki kuamini katika hili ila kunawanao tumia kalamu kama chambo cha kuwapata kimapenzi wale wanao wataka.sina ushahidi sana wa hili lakini habari zisizo rasmi ni hizo. sikiliza baadhi ya maoni na malalamiko kutoka kwa wanachuo mbalimbali pamoja na wale waliopitia katika elmu hii kwa kubofya hapa.

Nawapeni pole wale wote walio wahi kwa makusudi kabisa kufelishwa katika masomo yao.naamini ridhiki ya mtu haipotei ila inacheleweshwa tu, pia kwa wale wazembe katika masomo yao nawashauri mkaze buti na muache kupakaza kama nanyie ni miongoni mwa waathirika wa ufisadi huu.

vyuo vikuu bora Afrika.Afrika kusini yaongoza kwa ubora wa vyuo vyake

The InternetLab Ranking of 30 Top African Universities
Rank University Country World Rank

1 University of Cape Town South Africa 398
2 Universiteit Stellenbosch South Africa 566
3 Universiteit van Pretoria - University of Pretoria South Africa 718
4 University of the Witwatersrand South Africa 720
5 Rhodes University South Africa 738
6 University of South Africa South Africa 1,449
7 University of the Western Cape South Africa 1,553
8 American University in Cairo Egypt 1,826
9 Noordwes Universiteit - North West University South Africa 1,857
10 University of KwaZulu-Natal South Africa 2,214
11 University of Johannesburg South Africa 2,323
12 University of the Free State South Africa 2,369
13 Université de La Reunion France 2,387
14 Nelson Mandela Metropolitan University South Africa 2,542
15 University of Dar Es Salam Tanzania 2,819
16 University of Zimbabwe Zimbabwe 3,072
17 Al Akhawayn University in Ifrane Morocco 3,174
18 Cape Technikon South Africa 3,414
19 University of Mauritius Mauritius 3,682
20 University of Zululand South Africa 3,724
Source: InternetLab (Observatorio de Ciencia y Tecnologia en Internet)

------------------------------------------------------------------------------------^^^

Saturday, January 24, 2009

UMEME UMEKATIKA

SINA BUDI KUFUNGA VIRAGO VYANGU NAKUONDOKA KATIKA KITI CHANGU BAADA YA UMEME KUKATIKA NA SASA NATUMIA CHARGE KIDOGO ILIYOBAKI KUWAAGA.

LAKINI NINANI WA KULAUMIWA?
KUKATIKAKATIKA KWAUMEME LIMEKUWA NIJAMBO LISILO LA AJABU SASA SIJUI NI KWETU TU MOROGORO AU NA MIKOA MINGINE MNAPATWA NA HADHIA HII.
UMEME UNAKATWA KILA DAKIKA NA HAKUNAMAELEZO WANAYOTOA ILI NASISI WATUMIAJI TUWETUNAJUA NI MIDAGANI TUNAWEZA FANYA NINI! NI HASARA NYINGI TUNAZIPATA LAKINI HATUJUI NINANI TUMPELEKEE MALALAMIKO YETU NASERIKALI IMEKAA KIMYA KWAHILI!

ALARM ZIMEZIDI KWAHERINI JAMANI!

kumradhi

kutokana nasababu zisizokuwa ndani ya uwezo wangu nimekuwa nikikosekana katika kuendeleza libeneke la bloging, nimekuwa natatizo la log in kwenye blog yangu na hivyo kushindwa kufanya chochote, sijajua tatizo hili ni mimi pekeyangu ninalo au kuna ambaye lishamkuta ila hata hivi sasa imenibidi nitumie njia mbadala kuweza kuingia ndani ya nyumba yangu, inawezekana nimeingia kupitia dirishani hilo niachieni vile vile kwamuda wote nilikuwa nje ya nymba yangu nilikuwa napendelea kuchezea katika kijiji cha jirani na naamini hata wewe huna budi kukitembelea karibu sana hapa vile vile kuna kijiji cha wenzetu kina kwenda kwa jina la bongo yetu huna budi napo kukutembelea nisehemu nzuri pia za kushinda utakapo mapumziko.

namwomba mungu mlango wangu upone ili niweze rejea tena kwa kasi mpya katika nyumba yangu. poleni sana wote mlionitembelea nakukuta mlango umefungwa na sauti za popo na buibui kutawala katika nyumba yangu. natumahi nimerudi sasa