Wednesday, September 20, 2006

MR EBO ALISEMA MBADO HAJAWAI KUONA



self conteiner ndani ni choo cha shimo...mbado! kondoo a
naye rembua!!! mbado!!!!!!! sasa hiyo cha mtoto. umewahi kuona karoti yenye mahips? na bata akimpanda kuku? basi leo ona hiyo!!!!!!!!!!!!!

SABABU ZA TSUNAMI INASEMEKANA NI HAWA APA


KUTOKANA NA UZITO KUPITA KIASI INA SEMEKANA WALICHANGIA KUTOKEA KWA TSUNAMI, JE WEWE UNAUNGA MKONO????

Thursday, September 14, 2006

hii ni zaidi ya mapanki

tulivyoambiwa tunakula mapanki tulikataa na kumlaani hurbet sauper lakini minaona hii ni kashfa mbaya zaidi ya mapanki, mwenzangu unasemaje apo?

aliye kuja miaka ya tisini hata amini, miaka kumi ijayo mambo yatakuwaje?

Jamani eh,
Hivi kuna mtu ashawahi kukaa na kufikiri miaka michache ijayo mambo yatakuwaje??? Hebu kwa mfano mwaka 2016 twaweza shuhudia yafuatayo hapa Tanzania:
1) Wakati huo dawa ya ukimwi ishapatikana, mtu unaenda ofisini baada ya kutokuwepo kwa takriban majuma mawili. Bila shida unaongea na bosi wako huku ukimueleza..."Bosi, yaani ka-ukimwi kalinitandika vibaya sana last week" halafu sijui kwa nini mimi kananiandama hivyo.................

2) Bungeni napo tunakuwa na waheshimiwa kama Mr Ebo,
Kingwendu, Bambo na wafananao na hao. Unasikia spika akisema....Mheshimiwa Bambo swali la nyongeza. Bambo, "Mheshimiwa spika pamoja na majibu mazuri ya Waziri wa michezo na utamadun (Chifupa enzi hizo) naombi kuuliza swali hivi kwa nini siku ya fiesta isiwe sherehe ya kitaifa ambapo raisi atatoa mapumziko nchi nzima???

3) Uswahilini nako kama Manzese kutakuwa na maghorofa ya kutisha...Majungu ya akina mama wa apartment zilizo jirani yatakuwa...Hause girl wangu siku hizi hapiki bila kutizama DSTV ili kuona wenzake wa Afrika Kusini wanavyotengeneza masalo. Wewe wako bado anatizama kipindi cha mapishi ya ITV na Clouds TV???? Tv ya Clouds wakati huo kama CNN

4) Nako maofisini itakuwa utata mtupu, haitokuwa jambo la ajabu kuongea na bosi wa kiume huku heleni zinamning'inia masikioni. Na si ajabu akipata taarifa ya ghafla kuwa kampuni yake imepata hasara suruali ikamdondoka manake uvaaji ni ule wa bila mkanda huku ikiwa imeegeshwa chini ya matako (kata-K)"au nusu mlingoti"

5) Ukipita Sinza ndo utatoa macho...watoto wa chekechea wamajipanga kwenye ATM mashines kuchukua pesa ya kununulia lambalamba shuleni kwao. Yaani itakuwa mtafaruku mtupu...Mara mtoto mmoja anamwambia mtoto mwenzie, baba kanidipositia cheki feki, imebaunsi hivyo leo ice cream nitachukua kwa overdraft.

kikwete akichukua uzoefu kwa maveterani

Atawazee wakikutana mahali awakosi utani, hapo wanaonekana maraisi wastaafu mzee ruksa, ukweli na uwazi na kasi mpya wakibadilishana mawazo, maneno yaliopo chini yasichukuliwe maanani ni utani tu uliopandikizwa.