Saturday, November 18, 2006

Mkoa mpya wa magereza Tanzania


ule mkoa ulio ibuka Tanzania hivi majuzi umeweka sheria mpya za barabarani, mkuu wamkoa wa magereza bwana dito na kamanda wake wa mkoa bwana Zombe wametia saini kupitisha sheria hizo, baathi ni kama hiyo apo juu.

Wednesday, November 08, 2006

nafasi za kazi bongo


muliopo ugaibuni rudini bongo kuna nafasi nyeti za kazi, mwingine ndio huyo kajiachisha, mtoto wamjini Dito, naogopa wasije waka m Sadam, ingawaje sadamu hawakumtendea haki

wametuletea kachumbari sasa



mambo yamekucha bongo, kwa huduma za mawasiliano bongo inakuja juu, kama uliondoka miezi michache iliyopita ukija utabaki ukishangaa mambo kiulayaulaya, walitupatia huduma za GPRS kwenye simu zetu tigo na celtel,tigo na maanisha iliyokuwa ikiitwa mobitel tz,tunaweza kupata huduma za internate kwa kutumia simu na zaidi wamekuja jamaa wa kachumbari watembelee uone vinogesho kwa watumiaji wa simu za mikononi.achana na hao wale watafuta vipaji vya fleva za bongo Egidio najua unamkumbuka mkandiaji wa sanaa za bongo sister duu Salama, c ndiyo? watembelee bongo star search, wajamaa wanaponda hawa balaa, wengi wamejuta kushiriki, salama kama kawa anawapa za uso,ina discouradge lakini tutafika. pongezi kwa Master J kwa ushauri unaotoa kwa vijana iyo ndio inatakiwa, big up man!!!!!!!!!

SIFA ZA KIJINGA!!!!


Sii MABUZI tena, sasa ni ATM


Nazungumzia jina jipya kabisa la wanaume wakware maarufu kwa kuhonga zamani wakiitwa mabuzi sasa hivi ATM. ATM ni mashine maalumu za benki za kutumia umeme ambazo hutumika kuchukulia fedha saa yoyote na mahali popote ilipo, ilimradi una akaunti na kadi husika. Nilikuwa kwenye bar moja marufu hapa town na jirani yangu walikaa wanawake wawili wakiwa wanakunywa maji ya chupa kwa muda mrefu. wenyewe wanayaita maji spesho! Kwa mtazamo walionekana mambo yao si ”haba” (wanazo) na maana mavazi yao tu yalikuwa utambulisho kuwa wanapesa. lakini kwa kuwa nilikuwa karibu yao, niliweza kunasa mazungumzo yao kwa urahisi. ”Shoga hapa mimi nina elfu moja tu, tuagize maji ya mia tatu chupa mbili ili ibaki nauli, maana hii ATM yangu isipotokea tumeadhirika”, mwana dada mmoja alimweleza mwenzake.
Mashine ya ATM inayotoa fedha chapchap Nikajiuliza ATM wanayozungumzia hapa ni nini?nikasema leo nitaona mwisho wake.Nikajisogeza karibu yao kwa chat ili kunasa stori zaidi Haikupita nusu saa ilikuja gari moja ndogo na baadaye akashuka jamaa mmoja hivi akuonekana ameshiba sana,hapo ndipo mmoja kati ya wale wakina dada akaruka kwa furaha na kumwambia mwenzake ATM yangu hiyo sasa nina amani. Hapa ndiyo nikapata picha kuwa kumbe ATM inayozungumziwa hapa ni mwanaume! kweli baada ya jamaa kufika na kujiunga kwenye meza yao, meza yao ilibalika na kuwa ya ”heshima”, maana walianza kuagiza bia kwa fujo. Hapa najaribu tu kuwa kumbusha wale ndugu zangu ambao huwa wanajisahau sana kufanya mambo ya msingi na kuishia kuhonga zaidi kuwa sasa wamebatizwa jina jipya kutoka MABUZI na kuwa ATM. bwana egidio wahindi awajakugeuza ATM?