Friday, September 28, 2007

bongo forum

inawezekana umekuwa ukingojea hoja mbalimbali nzito ziihusuyo nchi yetu kwa kusubiri magazeti ya kuhabarishe, kama ujuavyo vyombo vya habari kama magazeti,radio na television vipo sana sana kwa kufanya biashara hivyo vimekuwa vikiangalia ni upande upi viegemee ili viweze kuuzika,vile vile kutokana na ushabiki wa baadhi ya wahandishi au itikadi zao za kisiasa vimekuwa vikitoa habari pasina uwazi unao takinika kwa kuhofia kushtakiwa au kufungiwa kujihusisha na masuala haya ya habari.
kukua kwa teknologia ya habari haswa kwa njia ya mtandao kumeleta fursa ya wanahabari wenye uchungu wa nchi yao kuweza kutoa habari bila ya mipaka ya kuofia chochote kuzuiliwa kwa njia yeyote.
nakumbuka dr slaa alipotoa majina ya walanchi magazeti mengi hayakuweza kumnukuu dr slaa na kutuacha hewani bila ya kututajia majina ya walanchi kama alivyo yataja dr slaa pale jangwani,
kwa mara ya kwanza nilikuja kuyaona majina baada yakupitia blog ya bwana Ansbet Nguruma
sasa basi labda ni usha mba wangu au sijui nijiiteje kwa kuchelewa kuujua mtandao wa bongoforum sasa kama nawewe ujawahi kuupitia jaribu leo naamini utakuwa hubanduki apa

Tuesday, September 18, 2007

did you know?

pitia hapo ujue zaidi

Monday, September 10, 2007

Wadau wa kitanzania wanaosaka nondo nchini Algeria




hawa ni jamaa kutoka bongo waliopo algeria wakisaka nondo za udaktari wa binadamu. wanafurahia baada ya kutembelewa na waziri wa sayansi technologia na elimu ya juu Bwana peter msolwa hayupo pichani.mliopo ughaibuni utajiskiaje waziri wako wa nchi anapokuja kuwajulia hali ilihali mpo ugenini? bwana Egidio ingekuwa wewe ungejiskiaje kumwana waziriwako wa elimu anakutembelea chuoni apo india?

Friday, September 07, 2007

Bithaa kutoka China





jamani kuna tetesi kuwa baadhi ya bithaa kutoka china zipo sokono kwa behi rahisi lakini inasemekana zina madhara kwa afya ya binadamu kitururu kaliongelea hili, Wito wangu kwa watanzania tushtuke kabla majanga haya ya kutengenezwa na wenzetu hayajatukuta

Monday, September 03, 2007

ivi ni kweli huu ndio ugonjwa ulio muua dada amina?

Ugonjwa huu mpya ambao aliugua Bi. Chifupa na uliosababisha mauti yake kwa
jina la kitaalamu hujulikana kama Uumbuajiasis Viongozitanzanialitis Hadharanium.

Ugonjwa huu unatokana na kufuatilia mambo ya serikali na viongozi kwa karibu kiasi cha kutaka kuweka ubovu wao hadharani.

Dalili kuu za ugonjwa huu ni hizi:

1.Kupenda nchi zaidi kuliko chama

2.Kuwa tayari kutetea mali ya Taifa na kuilinda mali hiyo

3.Kutoogopa yatakayokukuta

4.Kuanza kuweka hadharani ubovu na siri za viongozi hasa kwa jamaa yako wa karibu

5.Kutosikiliza ushauri wa kutakiwa kukaa kimya na wakubwa wako

6.Kuwa kimbelembele kuzungumza na kukemea maovu kila upatapo nafasi

7.Kuwa mtetezi wa Katiba na mkosoaji wa jamii

8.Kutolegeza msimamo hadi kifo.

Maambukizi:
Ugonjwa huu unaambukiza watu wachache kwani watu wengi wameshapatiwa kinga yake. Kwa wale wanaombukizwa wanafanya hivyo zaidi kwa kusoma habari za ufisadi, rushwa, na ubadhirifu katika serikali yao. Kwa kupitia mitandao, vitabu, na vyombo vya habari virusi vya ugonjwa huu vinajipenyeza katika akili za watu na kusababisha kusisimka kwa ubongo. Wale waliombukizwa ugonjwa huu hujikuta wakitafuta habari za kila namna na kushiriki mijadala yenye kutafakari mustakabali wa Taifa lao.

Kinga:
Ugonjwa huu kinga yake kubwa hujulikana kwa kitaalamu kama Mrungura. Kinga hii hutolewa kwa wale wote wenye kuanza kuonesha dalili za kukumbwa na ugonjwa huu. Kinga hii huwekwa kwenye mabenki na maofisi mbalimbali ili kuzuia viongozi wakubwa wasipatwe na virusi vya ugonjwa huu. Kinga hii pia hufanya kazi kwa wale walioanza kuonesha dalili kama kina Phillip Marmo, Chrisant Mzindakaya n.k Pindi mtu akishapatiwa kinga hii HAWEZI kuipinga serikali!

Tiba:
Hadi hivi sasa ugonjwa huu hauna tiba ya uhakika kwani wale ambao wameshaugua kwa muda mrefu hawako tayari kutibiwa kwani wanaona wanaishi vizuri tu na ugonjwa huu.

Karantini:
Pindi baadhi ya wakubwa wakiona kuna mtu ambaye amefikia hatua ya juu kabisa ya ugonjwa huu basi kwa mbinu wanazozijua wenyewe wanamkarantini, na wakati mwingine anakuwa katika hali hiyo ya kutengwa hadi kifo ili asiendelee kuwaambukiza watu wengine.

Tahadhari:
Kwa vile ugonjwa huu ni wa hatari, watu wabadhirifu, wezi wa mali ya umma, walaghai, na mafisadi hawawezi kuustahimili. Ugonjwa huu ni kinyume kabisa na watu hawa hivyo kamahutaki kuambuzizwa hakikisha unaendelea kujikita katika katika vitendo viovu vya kuharibu mali za umma na kuivunja vunja nchi huku ukishiriki katika kumegeana hadhina ya Taifa. Kwa vile ugonjwa huu unaendelea kuambukiza taratibu, kuna kila dalili hapo ulipo UNAISHI NA MUATHIRIKA