Wednesday, October 31, 2007
NILIKUWA KWENYE MAOMBOLEZO
ingawa sikuwashirikisha lakini sivibaya kama mkijuwa kwamba nilikuwa kwenye maombolezo ya rafiki yangu mpendwa na dada yangu kipenzi prisca Nkanyila aliye fariki kwa matatizo ya figo. ni kifo ambacho kimeniuma sana ukizingatia alikuwa bado mschana mdogo ambaye taifa lilikuwa likisubiria mchango wake.vilevile ni pigo kubwa kwa familia yake ukizingatia baba yake mzazi mzee nkanyila alifariki miezi miwili iliyo pita. alikuwa mwaka wa pili katika chuo kikuu cha ushirika moshi. pamoja na kugharimu figo yamdogo wake na kupelekwa matibauni nchini India bado mungu alimuhitaji zaidi. niliahidi kuiweka picha ya prisca nkanyila hapa sasa sikufanikiwa kuipata aliyo piga mwenyewe.kwa kumtambua prisca ni aliye vaa blauz ya bluu au wa3 toka kulia.
Subscribe to:
Posts (Atom)