Wednesday, October 31, 2007
NILIKUWA KWENYE MAOMBOLEZO
ingawa sikuwashirikisha lakini sivibaya kama mkijuwa kwamba nilikuwa kwenye maombolezo ya rafiki yangu mpendwa na dada yangu kipenzi prisca Nkanyila aliye fariki kwa matatizo ya figo. ni kifo ambacho kimeniuma sana ukizingatia alikuwa bado mschana mdogo ambaye taifa lilikuwa likisubiria mchango wake.vilevile ni pigo kubwa kwa familia yake ukizingatia baba yake mzazi mzee nkanyila alifariki miezi miwili iliyo pita. alikuwa mwaka wa pili katika chuo kikuu cha ushirika moshi. pamoja na kugharimu figo yamdogo wake na kupelekwa matibauni nchini India bado mungu alimuhitaji zaidi. niliahidi kuiweka picha ya prisca nkanyila hapa sasa sikufanikiwa kuipata aliyo piga mwenyewe.kwa kumtambua prisca ni aliye vaa blauz ya bluu au wa3 toka kulia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
10 comments:
Mkuu nilipata haabri hizi kwa masikitoko makubwa sana.
Namkumbuka sana Prisca.Alikuwa mpole,mtulivu asiekuwa na makuu.Nakumbuka siku 2 kabla ya kuja huku nilikuwa nae.
Nakumbuka aliweza kunipa moyo ushauri kwa baadhi ya mambo fulani.
Kweli tutakukumbuka Prisca.RIP
ni kweli tulimpenda lakini ngoja tuamini kwamba mungu alimpenda zaidi, kama unakumbuka alikuwa best wa mystella wangu,alikuwa mpatanishi wa viuzushi vya hapa na pale vilivyokuwa vikijitokeza enzi zile tukiwa muccobs, alikuwa mdogo mkiumri lakini mwingi wa busara na ushauri ambao naamini umlinisaidia na kufanikiwa kupunguza masa...nga. unakumbuka egidio? mambo ya royal
kaka asanteni kwa ushirikiano, hii inanipa moyo kwamba masela 2ko 2gether katika msiba wa rafiki yangu mpendwa Prisca E. Nkanyila. niwagusie kitu kimoja, mpendwa wetu Prisca alifariki siku aliyozaliwa. Niko katika kipindi kigumu sana kwani Prisca alikua mtu wangu wa karibu sana na mshauri mzuri sana ktk maisha, najaribu kujiuliza mtu anapokufa tunasema kazi ya Mungu haina makosa, je Mungu anaua? tuwe pamoja masela wangu. asanteni.
philipo naona umeamua kuji anony lakini tupo pamoja kaka! kazi ya mungu haina makosa, nilikuwa sijui kama birth day yake ndo imekuwa derth day yake
Poleni sana !
tunashukuru kaka kitururu kwa kutupa pole. tupo pamoja
Poleni sana..
damija fungate limeisha?
tunashukuru kwa kuwa pamoja, ahsante sana tumeshaanza kupowa
Poleni sana kwa kutanguliwa na ndugu yenu. Tuko pamoja.
Polleni sana.
Mama Malaika
Post a Comment