Wednesday, September 07, 2005

Hatari za kupiga simu kwa more subscribers

Jamaa mmoja ambaye ni mkurugenzi wa kampuni moja kubwa
ya mawasiliano alikaribishwa kutoa speech katika
tamasha moja la vijana lililokuwa limeandaliwa kuhusu
kujiepusha na vitendo vyenye kuweza kusababisha
maradhi ya kisasa.Speech ya mkurugenzi huyu
ilinukuliwa kama ifuatavyo;

Hali ni ngumu sana vijana kwa sababu kila mmoja
anataka kuonja uzuri wa maisha ya kisasa. Mtandao wa
ugonjwa huu ni mkubwa,mimi nashauri muwe makini .
Jitahidini sana kukaa bila kupiga.

Ni muhimu simu zenu mzitunze sana na wala si kupiga
piga kwani hii gharama yake ni kubwa.Kama shida ya
kupiga itakuwa kubwa, basi hakikisha simu yako iko
kwenye kipochi, na hivi vinapatikana kwa wingi na
gharama yake si kubwa.Hii inasaidia kupunguza
uwezekano wa kupata madhara yanayoweza kupatikana
kutokana na mionzi iliyoko katika simu hizi za kisasa.

Ni mwiko kabisa kupiga Voda kwa Voda kwani hii ina
hatari kubwa mno.
Watu wengi simu zenu zina fanya kazi vizuri tu na mna
hamu angalau ya kupibu, lakini hii nayo ni hatari,
kwani mwenzako akionyesha utashi wa kupokea ni rahisi
sana kwako kuamua kupiga kabisa.

Msifikiri mkikaa bila kupiga muda mrefu, eti simu zenu
zitamaliza chaji, hii si kweli.Hakikisha tu kwamba
simcard iko katika hali nzuri,hii ndio ina kumbukumbu
zote na ndio inaongoza mawasiliano yote.

Simu ni simu tu, na madhumuni yake yanafanana.
Usidanganyike na simu kuwa eti ina Kamera au double
skrini. Hizo ni mbwembwe tu.Kuna simu nyingi sana feki
siku hizi zinauzwa zimevishwa cover
mpya,usidanganyike.
Ukiona maisha bila kupiga hayawezekani, tafuta sehemu
inayoaminika na uwe unapiga hapo tu, hii inasaidia
sana kwani simu ukitumia peke yako inadumu zaidi
kuliko ile yenye subscribers wengi."

No comments: