Tuesday, September 06, 2005

UMEYASIKIA YA ARUSHA MAMBO YA WAWEKEZAJI AYO

Mwekezaji anapotoa kibano kwa Polisi
Meneja Mkuu wa zamani wa TanzaniteOne anayesota lupango baada ya kutoa mashambulizi na kibano kikali kwa OCD atapimwa kwanza akili yake kujua utimamu wa akili yake.

Mtuhumiwa huyo Joseph Kimble alitoa kibano cha aibu kwa kibosile wa polisi ambacho hakikutarajiwa baada ya Maafisa hao kumzukia katika Ofisi za mauzo ya tanzanite za Hakika Trading Company wiki iliyopita.

Kikosi hicho kikiongozwa na OCD Salawi kilitinga ofisi hizo katika shughuli za kikazi za kumkamata Kimble aliyekuwa anatuhumiwa kwa wizi wa tanzanite uliofanyika hivi karibuni mkoani Arusha.

Cha kushangaza Meneja Mkuu huyo wa enzi zake alianza kutukana matusi mazito mazito kwa Maafisa na jeshi letu la polisi na kuanza kumshambulia kwa kibano kikali OCD huyo na kumjeruhi vibaya.

Kibano hicho cha kudhalilisha jeshi letu kimekuja baada ya kuwepo malalamiko kibao ya Wabongo wachimbaji kusakiziwa mbwa na askari wa kampuni hiyo iliyowekeza katika madini ya Tanzanite na baadhi yao kupigwa risasi.

Kamanda wa Polisi Arusha James Kombe ametonya kuwa mtuhumiwa atapimwa akili kwanza kabla ya kuburuzwa mahakamani kujibu maswali namna alivyodiriki kurusha ngumi na kickboxing kwa maafisa wetu wa Polisi.

Na kama alidiriki kumtia kibano polisi, alikuwa anawafanyia nini wafanyakazi Wabongo enzi hizo akiwa ofisini?

No comments: