Friday, September 05, 2014
1. Maisha yako yanaweza kubadilishwa kwa muda mfupi na mtu hata usiemjua.
2. Watu wenye furaha pengine hawana kila kitu cha kuwapa furaha ila kile kidogo walichonacho hukipa maana ya kukifurahia.
3. Wapenzi wawili wanapogombana haimaanishi hawapendani,vivyohivyo wasiogombana haimaanishi wanapendana.
4. Unaweza kufanya jambo fulani la muda mfupi lakini likakunyima furaha milele .
5. Unapoagana na uwapendao waache na maneno mazuri pengine inaweza kuwa mara yako ya mwisho kuwaona.
6. Inaruhusiwa kuwa na hasira ila haimaanishi uwe katili.
7. Ukomavu wa mtu huja kutokana na changamoto alizozipitia kwenye maisha na kujifunza kupitia changamoto hizo na sio umri aliouongeza.
8. Wakati mwingine inatosha kusamehewa na wengine,ifike mahali ujifunze kujisamehe mwenyewe.
9. Sio lazima uwe na kiherehere cha kujua siri flani pengine kuijua kunaweza kubadili maisha yako milele.
10. Watu wawili wanaweza kutazama kitu kimoja lakini kila mmoja akaona tofauti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment