Wednesday, May 30, 2007
Wabongo tunatoka tu!!!!!!!!!
hatimaye mlimbwende wa Tanzania kwenye kinyang'anyiro cha kumtafuta mlimbwende wa wa dunia {miss universe 2007} ametutoa watanzania na waafrika kwa ujumla, kuwa baina ya walimbwende kumi bora duniani si jambo la kupuuzia ni jambo la kumpongeza na kumtakia mafanikio katika fani hii ya ulimbwende, ingawaje katika mahojiano aliyofanya kule mexico alisistiza kuwa ndoto zake ni kuwa injinia si kumbuki wa fani gani, hongera sana Flavian Matata, tunategemea utazidi kung'ara na kutupaisha katika anga za kimataifa ukishiriana na waliokutangulia.naamini ulistahili kufika zaidi ya hapo.habari zaidi bofya hapa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment