Wednesday, July 25, 2007

duh mambo manane musiyoyajua kuhusu mimi

kaka kitururu kani tag na kaniomba mambo nane muhimu wasiyojulikana kuhusu mimi.
labda la kwanza nihili na ingawa silipendi lakini ninalo, sijui kukasirika ingawa nauzika,kuonyesha hali ya kukasirika nashindwa nabaki naumia moyoni.
napenda muziki, napenda kuimba ila siwezi kushika mashairi,
napenda usingizi ila sipendi kulala,
sipendi kung'atwa na mbu ila ni mvivu wa kushusha net,
nina huruma sana,
kupiga kibuti siwezi, napataga shida sana hapa ila napenda kukutanamarafiki wapya,
napenda sana pombe ila sipendi kulewa,
napenda kuandikiwa barua , sms kwenye simu ila mvivu kujibu.
ayo ni baathi tu ya yale ambayo amyajui kuhusu mimi, ok namimi naomba niwakandamizie na mimi nana watuambie mambo nane tusiyo yajua kuhusu wao
wa kwanza ni
1.mjegwa
2.mwaipopo
3.chedieli
3.luihamu
4.damija
5.chemi chemponda
6.da'mija
7.father kidevu
8.miruko
nawasubiria kwa hamu wandugu!

4 comments:

Simon Kitururu said...

Unapenda usingizi lakini hupendi kulala! Duh!
Nahisi ukimchoka Zubeda mpaka ajue hutaki kuendelea naye ni miaka!:-)

chemshabongo said...

ndio kaka lakini kuna mistake nilifanya wakati na edit url sasa ikatokea kama unavyoona, nitafanyia marekebisho. lakini kuna hili nikushirikishe, jana wakati na post hiyo habari kuna dada akapitia nyuma ya computer yangu bahati akaona picha yako uliyoweka kwenye blog yako, akashtuka akanambia oh! huyu ni kaka kitururu mpare mmja tuliishi jirani mitaa ya forest enzi hizo akatimkia ughaibuni, alifurahi kukuona na anakusalimia sana. anaitwa grace masawe tupo naer kwenye iki kiofic tunapunguza muda wa kukaa duniani

Simon Kitururu said...

Msalimie Grace. Kama unayopicha yake anavyoonekana siku hizi itakuwa poa sana kuiona. Kweli dunia kiwanja kidogo.

Egidio Ndabagoye said...

Iyo ya pombe imenikumbusha mbali saaaana mkuu.