kutokana nasababu zisizokuwa ndani ya uwezo wangu nimekuwa nikikosekana katika kuendeleza libeneke la bloging, nimekuwa natatizo la log in kwenye blog yangu na hivyo kushindwa kufanya chochote, sijajua tatizo hili ni mimi pekeyangu ninalo au kuna ambaye lishamkuta ila hata hivi sasa imenibidi nitumie njia mbadala kuweza kuingia ndani ya nyumba yangu, inawezekana nimeingia kupitia dirishani hilo niachieni vile vile kwamuda wote nilikuwa nje ya nymba yangu nilikuwa napendelea kuchezea katika kijiji cha jirani na naamini hata wewe huna budi kukitembelea karibu sana hapa vile vile kuna kijiji cha wenzetu kina kwenda kwa jina la bongo yetu huna budi napo kukutembelea nisehemu nzuri pia za kushinda utakapo mapumziko.
namwomba mungu mlango wangu upone ili niweze rejea tena kwa kasi mpya katika nyumba yangu. poleni sana wote mlionitembelea nakukuta mlango umefungwa na sauti za popo na buibui kutawala katika nyumba yangu. natumahi nimerudi sasa
No comments:
Post a Comment